Tunafanya nini?

Ushairi ni sanaa iliyoandikwa zaidi nchini Tanzania na inakadiriwa kuwa na mashabiki wengi zaidi ukilinganisha na tanzu nyinginezo. Ushairi unachochea na kuhamasisha washiriki kutoka katika makundi na jumuiya zote na kuwa kiungo muhimu cha kijamii. Kwa sehemu kubwa ushairi unashughulikia kivitendo masuala yote yanayohusu maisha ya kila siku na uhsiano wa watu walio katika makundi mbalimbali.

Wakati mashairi ya mdomo yapo takribani katika lugha zote za Tanzania, kwa sababu ya sera ya ukuzaji wa lugha na utamaduni inaelezea, mashairi mengi yaliyoandikwa yapo katika lugha ya Kiswahili. Mashairi ya Kiswahili, kwa kweli, yanaonyesha wazi kabisa maisha ya kitamaduni ya Watanzania. Pia huonyesha na kueleza kwa kina kabisa, hisia zao, maadili ya kidemokrasia na matarajio yao ya baadaye.

Mashairi mengi yanachapishwa katika magazeti - mara chache katika vitabu. Kwa makadirio yetu, si zaidi ya makusanyiko 5 ya mashairi ya Kiswahili yamechapishwa nchini Tanzania katika kipindi cha miaka 10 iliyopita! Hivyo washairi kwa ujumla, tofauti na wasanii wengine, hutoa kazi zao na maarifa bure.

Miaka kumi iliyopita Tanzania ilikuwa na Mfuko wa Utamaduni uliotumiwa kukuza wa ubunifu kati ya mambo mengine. Ilichangia vyema maendeleo ya vipaji vya washairi na maandishi, kwa sababu washairi wengine walipewa tuzo, na wengine walipata usaidizi wa kuwasaidia kuandika au kuchapisha kazi zao. Mashirika mengine, kama Umoja wa Waandishi (UWAVITA) na Halmashauri ya Kitabu Tanzania (BAMVITA) pia iliunga mkono kazi za mashairi. Kwa bahati mbaya, leo msaada huo haupatikani tena.

Ukosefu huu wa msaada kwa waandishi, hususani washairi, unaathiri vibaya maendeleo yao kama wasanii na maandiko ya washairi wa Tanzania. Uamuzi wa Gerald Belkin kuunga mkono jitihada za washairi wa Kiswahili katika kukuza sanaa hii umekuja katika wakati muafaka. Hata hivyo, Mfuko wa Belkin ni mdogo na hawezi kwenda mbali sana katika kukuza maelfu ya washairi wa Kiswahili wanaohitaji msaada. Kwa hiyo, msaada zaidi unahitajika kutoka kwa mashirika mengine na watu binafsi.